Jinsi ya ku-unlock modem na kuweza kutumia sim card yoyote | HUDI TRICKS

Habari msomaji wangu samahani kwa kutokuwa hewani kwa muda kidogo lakini hilo lisikuvunje moyo kwani harakati za kuambukizana ujuzi bado zinaendelea leo tupeane na hili la ku unlock modem ya kampuni yeyote.

 Kutokana na ukuaji wa kasi wa matumizi ya intaneti kumepelekea makapuni ya simu za mikononi kubuni matumizi ya modem kwa ajili ya kuweza kupata huduma ya intaneti.



Ingawa kuna makampuni mengi ya simu na kila kampuni ina modems zake na ushindani pia kuchukua nafasi yake kwa kila kampuni kuwa na huduma ya vifurushi vitakavyowavutia wateja. Suala la kujiuliza ni je, utakuwa na modem kutoka kila kampuni kwa sababu huduma zao zimekuvutia? Hapana, jambo la kuzingatia ni kuwa na modem moja ambayo itakuwezesha kutumia line yoyote.

Hapa nitakuelekeza kwa kutumia Huawei E173, fuata maelekezo kulingana na aina ya modem yako.

Jinsi ya ku-unlock Huawei E173 modem

Pakua programu wezeshaji iitwayo  Huawei ‘Mobile Partner‘ kwa ajili ya Windows OS kama unatumia Windows kwenye kompyuta yako. Baada ya kuopakua ‘right click’ kisha bofya ‘Run as administrator‘. Kisha fuata maelekezo mpaka mwisho na kuistall.

  1. Weka sim card kwenye modem ambayo ni tofauti na kampuni ya simu; kama ni modem ya Airtel weka sim card ya Tigo, Voda, n.k ila sio line ambayo ni kutoka kampuni hiyohiyo inazotoa modem unayotumia kisha subiri mpaka iwe detected. Usiinstall programu (mobile partner) iliyokuja na modem.
  2.  Pakua na kuinstall DC Unlocker ya hivi karibuni. Kisha ifungue na kuchagua ‘Huawei‘ pia, chagua ‘Auto detect(recomended)‘ kisha bofya kitufe cha kutafuta(search).

 Funga mobile partner pamoja na DC Unlocker kisha download Firmware toleo la hivi karibuni. Ondoa mafaili hayo katika mkusanyiko wa pamoja(zip) kisha right click kwenye setup na ifungue kama administrator. Install mpaka mwisho wa mchakato mzima wa installation.
 Restart DC Unlocker. Kisha ifungue na kuchagua ‘Huawei‘ pia, chagua ‘Auto detect(recomended)‘ kisha bofya kitufe cha kutafuta(search). 
 Ili kuweza kufungua modem yako inabidi ulipie pesa kidogo kama Tsh 9,000 kwa kutumia Paypal kisha bonyeza severs kuweza kuweka username na password ambayo utatumiwa kwenye email address yako.
 Bonyeza ‘Unlock‘ kisha chagua ‘Read Unlock Code and auto enter to modem‘ halafu bonyeza ‘Do job‘.
 Bonyeza sehemu ya kutafuta(search) kuhakiki kama modem yako imefunguka na utaona sehemu ya ‘Sim lock status‘ imeandikwa imefunguliwa (unlocked).

Kwa kufuata hatua hizo utakuwa umeweza kufungua modem yako na kuweza kutumia sim-card yoyote kwenye modem yako? Je, umefanikiwa ku-unlock? niambie katika comment.

A Place Where You Get All kinds Of Tips And Tricks.

Nipe maoni yako hapa chini

Facebook Blogger Plugin by Khalid Riyad
huditricks.blogspot.com

Post a Comment

 
Top